Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embaro yupo nchini kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku 3, kuanzia jana tarehe 21 hadi 23 Juni 2024. Ni ziara ya kwanza kwa Rais kutoka taifa hilo la Afrika Magharibi kuzuru Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje, ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Guinea Bissau.

Akiwa na mgeni wake leo, Rais Samia ameleza mbele ya Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Juni 2024, Miongoni mwa maeneo ya mazungumzo yake na Rais Umaro yaligusia masuala mbalimbali ya uchumi na kukuza biashara na makhususi kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo cha korosho. Kwa kuanza na utafiti ili kuongeza thamani na uzalishaji wa zao hilo.

Guinea Bissau ni mashuhuri duniani kwa uzalishaji na uuzaji wa zao la korosho, inakadiriwa kuzalisha wastani wastani wat ani 200,000 ya korosho kwa mwaka 2022, ni miongoni mwa nchi 10 bora kwa mwaka 2022 katika uzalishaji wa zao hilo.

Tanzania ambayo inazalisha wastani wat ani 250,000 za korosho, ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uzalishaji wa zao hilo duniani.

Ushirikiano huo unaweza kuleta tija nzuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu nzuri za kilimo cha zao hilo, namna ya kuongeza thamani,taarifa za masoko, bei, na mengineyo.